Revelation of John 20:7-10

Kuhukumiwa Kwa Shetani

7 aHiyo miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake, 8 bnaye atatoka ili kuyadanganya mataifa yaliyopo katika pembe nne za dunia, yaani, Gogu na Magogu apate kuwakusanya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga ulioko pwani. 9 cNao walitembea katika eneo lote la dunia, wakaizunguka kambi ya watakatifu na ule mji unaopendwa. Lakini moto ukashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza. 10 dNaye ibilisi aliyewadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti walikokuwa wametupwa yule mnyama na yule nabii wa uongo. Watateswa humo usiku na mchana, milele na milele.

Copyright information for SwhNEN